Donate
China inahusika na Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na Uvuvi haramu katika Ukanda wa Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi: Uchunguzi mpya
Apr 11, 2024

China inahusika na Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na Uvuvi haramu katika Ukanda wa Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi: Uchunguzi mpya

By EJF Staff

Meli za uvuvi za China zinashusika katika Uvuvi haramu na ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi zilizo Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi (SWIO), kinyume na madai ya China kuwa inasaidia Maendeleo endelevu na kuimarisha uchumi wa bluu katika ukanda huu, kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa leo na Environmental Justice Foundation (EJF). Wavuvi wote waliohojiwa na EJF ambao wamefanya kazi katika Meli za China katika ukanda wa SWIO, wamekumbana au kushuhudia aina fulani ya ukiukwaji wa haki za binadamu au Uvuvi haramu.

Meli za China za uvuvi wa kina kirefu (DWF) kwa sasa ndiyo kubwa kuliko zote duniani kukiwa na kuongezeka kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uvuvi haramu. EJF imefanya uchambuzi wa kina wa meli hizo za China kwa miaka sasa, na kuibua uharamu na ukiukwaji usioweza kupingika.

EJF imekuwa ikifuatilia meli za China tangu mwaka 2020, na kufanya uchunguzi kadhaa katika shughuli zake haramu na shughuli zisizo na maadili kwa kufanya mahojiano 318 na wafanyakzi wa zamani wa meli za China, ambapo kati ya mahojiano hayo, 96 ni ya miezi 6 iliyopopita. Hata hivyo, kiwango cha uhalifu katika ukanda wa SWIO unasimama kiyume kabisa na maslahi ya China yanayodaiwa katika ukanda huu. Uchunguzi huu mpya unaibua vifo vinne vilivyotokea katika meli za China kati ya mwaka 2017 na 2023, ikijumuisha mfanyakazi mmoja aliyedaiwa kujiua mwenyewe kwa kujirusha kwenye maji.

Ripoti hii imetokana na mahojiano na wafanyakazi wa meli za China katika Ukanda wa SWIO na taarifa nyingi kutoka kwa vyanzo vya pili vya taarifa na ndiyo ripoti ya kwanza kumulika shughuli za meli za China katika ukanda huu. Kati ya mwaka 2017 hadi 2023 meli za China zimehusishwa na matukio 86 ya uvuvi haramu au ukiukwaji wa haki za binadamu katika ukanda wa SWIO. Kati ya meli 95 za uvuvi wa jodari ambazo kwa sasa zimepewa ruhusa katika ukanda wa SWIO, karibu nusu yake zinajihusisha na matukio ya Uvuvi haramu na/ au ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kati wavuvi 44 waliohojiwa, 80% waliripoti ukataji wa mapezi ya papa, 100% waliripoti mazingira mabaya ya kufanyia kazi, 96% walikutana na muda mrefu wa kufanya kazi na 55% walikutana na ukatili wa kimwili. EJF ilihoji wavuvi 16 waliofanya kazi katika meli za China nchini Msumbiji ambao walieleza uharamu mkubwa, ikiwa ni 81% kukutana na ukatili wa kimwili na nusu yao wakishuhudia kuvuliwa kimakusudi na/ au kuacha na majeraha jamii muhimu za wanyama wa majini.

Vyakula vya baharini vinavyotokana na meli hizi zimeonekana kuingia katika masoko muhimu kimataifa kama Ulaya, Marekani, Japan, na Korea kusini: asilimia 73 ya meli zinazohisiwa kufanya ukiukwaji wa haki za binadamu na uvuvi haramu zilionekana katika meli zilizoruhusiwa kusafirisha samaki hadi Ulaya wakati ripoti hii inaandaliwa.

Kupitia mradi wake wa Belt and Road Initiative (BRI), China imewekeza vya kutosha katika nchi za Ukanda wa SWIO, ikiwa na pamoja na ujenzi wa bandari na miundombinu ya Uvuvi. Makubaliano ya uwekezaji huu mara nyingi siyo wa wazi, licha ya kuwepo kwa makala chanya kuhusu Uwekezaji wa China katika vyombo vya habari vya ndani, huku malalamiko yakiibuliwa na asasi za kiraia na jamii za maeneo husika kuhusu madhara ya uwekezaji huu kwa jamii za pwani.

Uchunguzi huu mpya unaonesha uwekezaji wa China kuwa mbali na kunufaisha jamii hizi, iwe moja kwa moja au vinginevyo uwekezaji huu unaathiri maisha ya wavuvi wa ndani kutokana na Uvuvi haramu unaofanywa na meli za China za uvuvi wa kina kirefu.

Steve Trent, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa EJF, anasema : “Utafiti wetu wa kina unaibua maswali rahisi : Je, Ukiukwaji huu ndio mwelekeo wa serikali ya Beijing, au ni kushindwa kwake kusimamia meli zake? Uzito wa ushahidi wetu unaonesha moja kati ya hivi ni lazima iwe ukweli.”

“Tumeibua kuwa Meli za Uvuvi wa kina kirefu za China (DWF) zinahusika na ukiukwaji wa kutisha na Uvuvi haramu katika ukanda wa SWIO. Kitu ambacho uchunguzi wetu unaonesha ni kuwa ukiukwaji huu haujafanywa na meli moja ; eneo moja la kijiografia; lakini meli zote za uvuvi za China katika maeneo yote tuliyoyochunguza.

Wakati serikali ya China ikionesha kuwa uwekezaji wake katika ukanda wa SWIO ni wa manufaa kwa pande zote, lakini Ukweli ulio dhahiri ni kuwa unaumiza eneo hili. Hii inajumuisha jamii za pwani ambazo maisha yao yanahatarishwa na meli hizi za kibiashara, watu wanaoteseka na ukiukwaji wa haki zao kati meli hizi na nchi za Ukanda wa SWIO zinazokumbana na rushwa na madeni kutokana na uwekezaji wa China.

“Ni muda sahihi sasa wa kuangalia kwa ukaribu meli za uvuvi wa kina kirefu za China ukiwemo uwekezaji wa China katika ukanda huu na Tume ya Jodari ya bahari ya Hindi (Indian Ocean Tuna Commission), nchi za pwani, nchi za masoko, nchi zinazomiliki bandari, nchi zenye bendera ya meli na zaidi ya yote ni Serikali ya Jamhuri ya watu China. Kwa kiwango cha chini, hii lazima ihusishe uwazi katika Uvuvi kuwezesha kila mtu kuelewa nani anavua, anavuaje, wapi, na kwanini. Meli za China za uvuvi wa kina kirefu (DWF), siyo watuhumiwa pekee wa Uvuvi haramu katika ukanda wa SWIO, lakini dhulma zake za kutisha zinazofanyika katika ukanda huu zinahitaji mabadiliko makubwa.”

MWISHO

Maelezo kwa mhariri

Soma ripoti kamili hapa na anagalia filamu hapa.

Kulinda utambulisho wa vyanzo vyetu, matukio ya meli binafsi za watu hayakuchapishwa lakini zitapatikana kwa maombi maalum.

EJF inafanya kazi kimataifa ikiangalia sera na kuchochea mabadiliko ya kudumu ili kulinda mazingira na kulinda haki za binadamu. Tunachunguza na kuibua ukiukwaji na kuwasaidia watetezi wa mazingira, jamii za asili na waandishi wa kujitegemea ambao wako mstari wa mbele katika kupinga uhalifu wa mazingira. Juhudi zetu zinalenga kupata amani, usawa na uendelevu.

Wachunguzi, watafiti, waandaji wa filamu na wanakampeni wetu wanafanya kazi na washirika wa ngazi za chini na watetezi wa mazingira kote duniani. Kazi yetu katika kupata haki ya mazingira inalenga kulinda hali ya hewa ulimwenguni, bahari, misitu, na wanyamapori na kulinda haki za msingi za binadamu. Kwa maelezo zaidi au kuongea na mmoja wa wataalamu wetu, tafadhali wasiliana nasi kwa media@ejfoundation.org